Monday, 11 December 2017

1. Ni tabibu wa karibu; tabibu wa ajabu;
na rehema za daima; ni dawa yake njema.

Imbeni, malaika, sifa za Yesu Bwana;
pweke limetukuka jina lake Yesu.
                     Hatufai kuwa hai, wala hatutumai,
                     ila yeye kweli ndiye atupumzishaye.

2. Dhambi pia na hatia ametuchukulia;
Twenendeni na amani hata kwake mbinguni.

3. Huliona tamu jina, la Yesu kristo Bwana,
yuna sifa mwenye kufa asishindwe na kufa.

4. Kila mume asimame, sifa zake zivume;
Wanawake na washike kusifu jina lake.


5. Na vijana wote tena, wampendao sana,
waje kwake wawe wake kwa utumishi wake.

1 comment:

Followers

Social Networks

Popular Posts

Blog Archive