Tuesday, 12 December 2017

Bwana Yesu asifiwe,

Wakati wa kuoa ni wakati wa ujana Mal 2:14 Biblia inasema mke wa ujana wako, hii inaonesha kibiblia wakati sahihi wa kuoa ni wakati wa ujana, hakuna wakati mwingine ambao ni sahihi sana wa kumpata mwenzi wa maisha isipokuwa ujanani.

Mtu wa kwanza kuwepo duniani ni kijana moja Adamu na mkewe Hawa ambao Mungu aliwapa maagizo ili wazae ili tuongezeke, Kabla hawajatenda dhambi Adamu anazungumza Utamwacha baba yako na mama yako utaambatana na mwenzi wako na mtakuwa mwili mmoja hata hakujawa na dhambi duniani.

Tunapozungumza suala la mahusiano ya kijana na Binti tunazungumzia suala takatifu kwasababu aliyelianzisha  wa tendo hili ni mtakatifu, ni sisi tumekuja kuingiza mambo mengi na kufanya suala hili kuharibika

Mahusiano  yanapitia hatua kadha wa kadha kama ifuatavyo:-
1.      Urafiki
Ni mahusiano ya kawaida ambayo kijana wa kiume na kijana wa kike wanaweza kuwa wanashirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii, kimasomo, kiuchumi hata kisiasa bila kuwa na agenda nyingine

2.      Uchumba
Ni mahusiano ya kijana wa kiume na kijana wa kike ambao wamekwisha peana ahadi ya kuoana. Katika hatua hii huwezi kumuita mchumba wako mke au mume.

Ni kipichi cha matazamio cha watu wawili wa jinsia ya kiume na jinsia ya kike kabla ya kuoana au kuna Ahadi ya kuoana, uchumba sio urafiki wala sio ndoa.

3.      Ndoa
Ni mahusiano ya kijana wa kiune na kijana wa kike ambao wamekwisha weka agano la kuishi kama mume na mke.

Kuna agano la watu wawili wa jinsia ya kiume na jinsia ya kike la kuishi pamoja kama mume na mke.

Mambo ya kuzingatia kwa kijana wa kiume kabla hujatafuta mwenzi:-

1.      Kumpokea yesu
Ukipatana na Mungu, Mungu Mungu atakusikiliza nawe utasikiliza, Ni vema kupatana na Mungu kwanza.

2.      Kufanya kazi
Usichumbie kama huna kazi, Mwa 2:8 Mungu alimuweka Adamu Edeni kwanza alime (Afanye kazi) ndipo alipo mletea mke (Hawa)Mwa 2:18 hivyo lazima ufanye kazi

3.      Kupata mwenzi
Mwa 2:18 Neno linasema “Bwana Mungu akasema,Si vema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana nae.”
Hata kama umewahi kukosea katika kufanya uchaguzi ikakupelekea kuumizwa bado una nafasi ya kuinuka tena Mit 24:16 “Bali mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya” Inawezeka na mpaka sasa umefikia mahali pa kuona wanaume wote ni maadui au wanawake wote ni maadui, hapana inuka tena Muombe Mungu huko upande wako atakusaidia, kwa kuwa anakupenda sana.

Zingatia mambo haya:
Mathayo 7:7  “Ombeni nanyi mtapewa; Tafuteni nanyi mtaona; Bisheni nanyi mtafunguliwa”

“Ombeni nanyi mtapewa”
Hii ni hatua ya kwanza, anza kwa kumuomba Mungu akupe mke mwema, mume mwema, mtangulize Mungu katika jamba hii, usimwendee mungu ukiwa tayari una majibu

“Tafuteni nanyi mtaona”
Wengi wameishia kwenye hatua ya kwanza ya kuomba wakaacha kutafuta, Baada ya kumpelekea hoja yako Mungu unataka mwenzi wa namna gani, tafuta ni hatua ya pili.

“Bisheni nanyi mtafunguiwa”
Sasa wengi wao hatua hii wanaiogopa ya kubisha hodi (Uthubutu) baada ya kuomba Mungu, ukatafuta kinacho fuata ni kuthubutu, Mwambie mimi nie……… nataka……… mwa 2:23 “Adamu akasema, sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamk, kwa maana ametwaliwa katika mwanaume”

Mungu akubariki sana   

Usiache kufuatilia:

Youtube       Facebook          Twitter



0 comments:

Post a Comment

Followers

Social Networks

Popular Posts

Blog Archive