Monday, 11 December 2017


1.Mwokozi umeokoa, nimekuwa wako wewe,
damu imenisafisha; sifa kwa mwana kondoo.

Utukufu, Aleluya! Sifa kwa mwana kondoo!
 Damu imenisafisha, utukufu kwa Yesu!

2.Nilijitahidi sana, ila sikupata raha,
bali kwa kumtegemea, nilipata Baraka

3.Daima namwegemea, damu ikifanya kazi,
nikioga kwa chemchemi, itokayo mwokozi.

4.Sasa ninewekwa wakfu; Nitaishi kwako wewe:
Fahari nashuhudia, ya wokovu wa bure.

5.Nasimama kwake Yesu, ameponya roho yangu:
ameniondoa dhambi, anifanye mzima.

6.Nilikuwa kifungoni, niliteswa na dhambi,
nilifungwa minyororo, Yesu akanifungua.

7.Sifa, ameninunua! Sifa, nguvu za mwokozi!
Sifa, Bwana huhifadhi! Sifa zake milele.

0 comments:

Post a Comment

Followers

Social Networks

Popular Posts

Blog Archive