Wednesday, 27 December 2017


Bwana Yesu asifiwe,

Yako mambo kadha ambayo ukiyachunguza unaweza kuutambua wito wako kwa haraka zaidi na kukuondoa kwenye sitofahamu ya wito wako. Watu wengi kanisani wanamtumikia Mungu chini ya viwango si kwasababu hawampendi Mungu ila kwasababu hawajajua wito wao kila kona utawakuta sikwamba wao ni kimbele mbele ila hawajajua ni eneo gani ambalo Mungu amewaitia ili wakae katika eneo hilo na kufanya katika viwango

Mf. Kuimba hupo, kufundisha hupo, kuhubiri yupo, kuonya yupo, kuchunga, kufariji yupo nk na vyote anafanya juu juu tu, si katika kiwango ambacho Mungu anachotaka, kwasababu hawajajikita kwenye wito wao.

Fuatilia zaidi ujifunze kwa kina namna ya kuujua wito wako kibiblia, kama ifuatavyo;-
  1. Amani na Furaha ya moyoni
  2. Kupenda na Kuridhika
  3. Kutumia Muda Zaidi
  4. Uwezo mkubwa ktk hilo
  5. Matokeo Mazuri
  6. Baraka na Mafanikio
  7. Ushuhuda mzuri wa wengine

Unaujuaje wito wako?.



1 Amani na Furaha ya moyoni
Isaya 55:12,
“Maana mtatoka kwa furaha, mtaongozwa kwa amani” katika kuujua wito wako jiulize maswali hay, Je! Hili ninalolifanya ndani yake ninapata furaha na amani au najilazimisha tu,
Filipi 4:4-7,
“Furahini katika Bwana siku zote; tena nasema furahini.  Na Amani ya Mungu ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu” katika mistali hii inaweza kukusaidia kujipima katika kila huduma unayoifanya je ni yako au ya mtu mwingine.
Unapotumika katika eneo hilo ndandi ya moyo wako kunajawa na furaha na Amani au unakuwa kawaida tu au unafanya kwa kusukumwa.
Kolosai 3:15
“Na Amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani” Je amani ya kristo ndani yako inaamua nini, Au jambo gani unapolifanya unasikia Amani katika Mungu.
Zab 16:11,
Kwenye wito wako lazima utapata furaha tele na mema


2.      Kupenda na Kuridhika
Kut 33:12-14
Mungu anamwambia Musa “Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha” kwamba katika wito huo hutanitumikia tu bali nitakupa raha. Moyo wako hautapungukiwa katika kufurahia wito wako, huta kaa ujute.
 Math 11:29-30
“Jitieni nira yangu” kuambatana na Yesu/Ukikaa katika wito wako “Nanyi mtapata raha nafsini mwenu” utapata raha. Ukiona unafanya huduma Fulani na katika hali ya kuifanyia kazi moyo wako haupokei kitu kwa Mungu jiulize Je! Huu ni wito wangu kweli au ni eneo linguine.


3.      Bajeti ya Muda zaidi
Katika eneo ambalo ni wito wako utaona jinsi unavyo jishughulisha na jambo hilo kwa muda mrefu kuloko mambo mengine.
Mf. Mkulima utamjua kwa jinsi anavyojishughulisha sana na kilimo, mfugaji atajihusisha sana na ufugaji kuliko kitu kingine, hilo tu ni kiashiria cha kuonesha kuwa mtu huyo ni wa namna gani
Kut 33:7-11,
Musa sikuzote alikuwa anabeba hema la kukutania na kuhudumu watu wa Mungu, kwasababu huo ndio ulikuwa wito wake. Mungu alimuita katika eneo hilo.
Je! Wewe ni utumishi upi unaokuchukua muda mwingi?


4.      Uwezo mkubwa wa Kazi hiyo
Mtu ambaye kaitwa katika eneo Fulani utaona uwezo mkubwa alionao katika kufanya jambo hilo.
Kutoka 31:1-5,
Mungu anamwambia Musa “ nimemwita Bezaleli, name nimemjaza Roho ya Mungu, katika hekima na maarifa, na ujuzi na mambo ya kila aina. Ili abuni kazi za ustadi……….” Bezeleli alikuwa na uwezo mkubwa katika hekima, maarifa na ujuzi vitu vilivyo onesha dhahili wito wake kwa Mungu
Matendo 6:7-10.
Stefano alikuwa na uwezo mkubwa katika kufanya maajabu na ishara kubwa, hii ilionesha wazi wito wake.
Jiulize wewe una uwezo mkubwa katika kufanya wito upi? Pia inawezekana ukawa na wito zaidi ya moja sio tatizo, muhimu kila wito Mungu aliouweka ndani yako uutumikie katika viwango ambavyo vinatakiwa.
5.      Matokeo Mazuri 
Kwenye wito huo unaotumika Je! Unapata matokeo gani? Mazuri au mabaya. Pia unaweza kukapata matokeo mabaya katika wito ambao ni wako kwasababu tu yakukosa maandalizi, kuishi maisha yasiyompendeza mungu nk.
Yohana 5:36,
Kazi unazozifanya na matokeo yake ndizo zikushuhudie kuwa wewe umeitiwa katika eneo gani
Marko 16:15-20,
“Na ishara hizi zitafuatana na…..” Matokeo ya mazuri ya kazi uliyoifanya ni dalili tosha ya kukujulisha wito wako.
Matendo 8:4-8.


6.       Baraka na Mafanikio
Unapokanya wito wako Baraka na Mafanikio lazima vikuambate
Zaburi 1:3,
“Nae atakuwa kama mti uliopandwa; kando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; na kila alitendalo litafanikiwa.”
 Mithali 10:22
“Baraka ya bwana hutajirisha, wala hachanganyi huzuni nayo” Katika eneo ambalo ni wito wako huwezi kuwa na huzuni bali utaambatana na Baraka tele katika wito huo.
Mith 17:8,
“Kipawa ni kitu cha thamani kwake yeye aliyenacho, kigeukapo hufanikiwa” kipawa ni wito wa mtu, anasema kila kigeukapo hufanikiwa”mtu akikifanyia kazi utafanikiwa, utapata mapokeo mazuri katika wito huo.


7.      Ushuhuda mzuri wa Watu wengine
Math 18:16,
“Zawadi ya mtu humpatia nafasi, humleta mbele ya wakuu” wito wa mtu unampatia mtu nafasi/kibali katika eneo la wito wake, kwasababu watu wanaona ni eneo gani ambalo wewe unafanya vizuri.
Yoh 3:1-2,
Nikodemu alimshuhudia Yesu kuwa ni nani, Alikuwa anaona kilichopo ndani ya Yesu
Mdo 6:1-8.
Mitume alichagua watu saba watakaosimama kwa ajili ya kutoa huduma kwa wahitaji kulingana na wito wao. Wito ndani mtu hauwezi kijificha labda mtu mwenyewe asitake kutumika.

Nimeeleza kwa kifupi tu vigengele kadha vitakavyo kufanya uweze kuutambua kwa haraka wito wako kwa Mungu ili usigongane na watu wengine katika wito wao. Bila kuzingatia hayo utajikuta kila siku unatumika chini ya kiwango kwasababu ya kutokaa katika eneo lako mpaka kufikia hatua ya kuona kama wokovu ni mzigo au hauna faida yoyote.

Mungu anakufundisha ili upate faida, Usiwe na utumishi usiokuwa na faida yoyote pia ujue namna ya kusimama katika wito wako

Mungu akutie nguvu katika utumishi wako


Mungu akubariki sana!

 Fuatilia zaidi masomo haya na mengine katika kitandao ya kijamii kama ifuatavyo;-
Blog:                    -        mungupendo.blobspot.com
Facebook:           -        Mungu Anakupenda
Youtube:              -        Mungu Anakupenda
Twitter:                -        Mungu Anakupenda



0 comments:

Post a Comment

Followers

Social Networks

Popular Posts

Blog Archive