Wednesday, 21 March 2018

Bwana Yesu asifiwe

Kuna siri kubwa imejificha katika tendo la msamaha, hebu tujifunze kwa kina siri hii huenda ikasaidia kuponya majeraha na machungu yaliyomo katika nafsi yako.

Yapo mambo kadha tunaenda kujifunza kama yafuatayo
1. Msamaha ni nini
2. Kwanini tusamehe
    3. Msamaha unafaida gani/ umuhimu gani
    4. Ninawezaje kusamehe
    5.  Nini matokeo ya kuto kusamehe

Msamaha
Ni tendo la kumuachilia mtu ambaye amekusababishia maumivu katika moyo wako, Ni tendo la kumuondolea hatia mtu ambaye amekufanyia mambo yaliyopelekea moyo wako kuumia/ kupata uchungu

Sala ya Bwana inasema “Utusamehe makosa yetu kama sisi tuwasamehevyo wanaotukosea” Kwanini Mungu akupe kusamehe kwanza ndo upate kusamehewa?

Msamaha ndio unaokupa uhai pamoja na Mungu, ule uhai ndio unaokupa wewe nguvu ya kusamehe wengine, wapo baadhi ya watu wapo tayari kufa kuliko kusamehe watu wengine, ni  ukweli wa ajabu japo msamaha ni mchakato mgumu na mgumu. Sio jambo linalofanyika usiku mmoja. Ni mageuzi ya moyo, ni neno ndogo na rahisi, lakini ni ngumu sana kumsamehe mtu ukiwa umeumizwa sana.

Kumsamehe mwingine hakufuti kumbukumbu za zamani za machungu uliyoyapata bali kunaondoa uchungu kupitia uponyaji unaotokana na tendo hilo la msamaha. Msamaha ndio unaokupa kibali mbele za Mungu, lazima ukubali gharama kusamehe ni gharama tena kubwa

Yapo mambo haya
1. Luka 17:3 “Jilindeni, kama ndugu yako akikosa mwonye akitubu msamehe”
Neno hili linaeleza habari  za kugawana gharama, kwanza kama ndugu akikosa mwonye, pili akitubu msamehe. Upo uwezekano wa mtu huyo kukataa kutubu Je? Asipo kubali maonyo unafanya nini hapo. Usisubiri kuombwa msamaha ndo usamehe.

     2. Warumi 5:8 “Bali Mungu aonesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwakuwa kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi”
Hii ni hatua kubwa ya msamaha ambayo kila mtu anatakiwa kuwa nayo, kristo alikufa kwa ajili yetu tukiwa tungali wenye dhambi, alitangaza msamaha kwetu tungali watendaji wa mambo yaleyale ambayo ni chukizo kwake

Usisubili kuombwa msamaha, eti hajaomba msamaha nimeshindwa kumsamehe, alitakiwa kuombe msamaha ndo nimsamehe, kama unasubiri kuombwa msamaha ujue kuuona ufamle wa mbinguni kwako itakuwa ngumu

Lazima ukubali kubeba gharama zako na za yule unaye msamehe, kumuonya aliye kokosea ni kutaka kugawana gharama ambazo ulitakiwa kuzibeba wewe mwenyewe. Ukijivika ujasili utaweza kusamehe

Msamaha ni tiba ya nafsi, hurejesha kila kilicho potea, huleta upatanisho, huondoa hukumu, hurejesha mahusiano yaliyo potea
 Zab 103 2-5 Akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhiri na rehema, aushibisha mema uee wako, ujana wako aurejesha kama tai.

Aliye kuumiza hawezi kukuondolea maumivu wala uliye muumiza huwezi kumwondolea maumivu, bali kristo mwenyewe ndani yetu ndiye awezaye kutuondolea maumivu, majeraha na machungu  iwapo tu utampa nafasi.

Tendo alilolifanya Yesu lilikuwa la kijasiri, hata wewe unaweza kuwa jasiri kama Yesu kwakuwa hupo ndani yako, mruhusu akusaidie kufanya maamuzi magumu.
 “Nayaweza mabo yote katika yeye anitiaye nguvu” Nguvu ya kusamehe  inattegemea maamuzi yako,  Vile unavyo amua kusamehe ndinyo Mungu anavyo kutia nguvu za kusamehe

Unacho hitaji ni kusamehe na kusahau bila kujali kafanya nini na ni nani na kwanini ili uishi maisha furaha, kusamehe ni uwezo wa kukubali ukweli wa mambo.

Kusahau ni kukubali, huwezi kusahau kile mtu alichokufanyia, lakini yote unahitaji tu kufanya ni kukubali ukweli kwamba uliopita umepita na kuondoa chuki hizo moyoni mwako.
Huna haja ya kusubiri au kusikia mtu anakuja kwako kuomba msamaha ili umsamehe. 

Haiwezi kamwe kuja. Hebu msamaha uwe maisha yako “Tabia yako” ambayo haitategemea tabia ya mtu mwingine, bali kwa moyo wako wa ukarimu.

Ebr 12:14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hakuna mtu atakaye muona Mungu asipokuwa nao. Kila mwenye matarajio ya kwenda mbinguni ni lazima  roho ya msamaha iwe maisha yake, Utaishi kwa amani, kwa furaha, hutakuwa nauchungu kamwe.

Fuatilia zaidi masomo mengine:-
Youtube         :           Mungu anakupenda
Twitter            :           Mungu anakupenda
Facebook       :           Mungu anakupenda

Followers

Social Networks

Popular Posts

Blog Archive