Bwana Yesu asifiwe,
Yako mambo kadha ambayo
ukiyachunguza unaweza kuutambua wito wako kwa haraka zaidi na kukuondoa kwenye
sitofahamu ya wito wako. Watu wengi kanisani wanamtumikia Mungu chini ya
viwango si kwasababu hawampendi Mungu ila kwasababu hawajajua wito wao kila
kona utawakuta sikwamba wao ni kimbele mbele ila hawajajua ni eneo gani ambalo
Mungu amewaitia ili wakae katika eneo hilo na kufanya katika viwango
Mf. Kuimba hupo, kufundisha hupo,
kuhubiri yupo, kuonya yupo, kuchunga, kufariji yupo nk na vyote anafanya juu
juu tu, si katika kiwango ambacho Mungu anachotaka, kwasababu hawajajikita
kwenye wito wao.
Fuatilia zaidi ujifunze kwa kina
namna ya kuujua wito wako kibiblia, kama ifuatavyo;-
- Amani na Furaha ya moyoni
- Kupenda na Kuridhika
- Kutumia Muda Zaidi
- Uwezo mkubwa ktk hilo
- Matokeo Mazuri
- Baraka na Mafanikio
- Ushuhuda mzuri wa wengine
Unaujuaje wito wako?.
1 Amani na
Furaha ya moyoni
Isaya 55:12,
“Maana mtatoka kwa furaha,
mtaongozwa kwa amani” katika kuujua wito wako jiulize maswali hay, Je! Hili
ninalolifanya ndani yake ninapata furaha na amani au najilazimisha tu,
Filipi 4:4-7,
“Furahini katika Bwana siku zote;
tena nasema furahini. Na Amani ya Mungu
ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu” katika mistali hii
inaweza kukusaidia kujipima katika kila huduma unayoifanya je ni yako au ya mtu
mwingine.
Unapotumika katika eneo hilo ndandi
ya moyo wako kunajawa na furaha na Amani au unakuwa kawaida tu au unafanya kwa
kusukumwa.
Kolosai 3:15
“Na Amani ya Kristo iamue mioyoni
mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani” Je
amani ya kristo ndani yako inaamua nini, Au jambo gani unapolifanya unasikia
Amani katika Mungu.
Zab 16:11,
Kwenye wito wako lazima utapata
furaha tele na mema
2. Kupenda na
Kuridhika
Kut 33:12-14
Mungu anamwambia Musa “Uso wangu
utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha” kwamba katika wito huo hutanitumikia
tu bali nitakupa raha. Moyo wako hautapungukiwa katika kufurahia wito wako, huta
kaa ujute.
Math 11:29-30
“Jitieni nira yangu” kuambatana na
Yesu/Ukikaa katika wito wako “Nanyi mtapata raha nafsini mwenu” utapata raha.
Ukiona unafanya huduma Fulani na katika hali ya kuifanyia kazi moyo wako
haupokei kitu kwa Mungu jiulize Je! Huu ni wito wangu kweli au ni eneo
linguine.
3. Bajeti ya
Muda zaidi
Katika eneo ambalo ni wito wako
utaona jinsi unavyo jishughulisha na jambo hilo kwa muda mrefu kuloko mambo
mengine.
Mf. Mkulima utamjua kwa jinsi
anavyojishughulisha sana na kilimo, mfugaji atajihusisha sana na ufugaji kuliko
kitu kingine, hilo tu ni kiashiria cha kuonesha kuwa mtu huyo ni wa namna gani
Kut 33:7-11,
Musa sikuzote alikuwa anabeba hema
la kukutania na kuhudumu watu wa Mungu, kwasababu huo ndio ulikuwa wito wake.
Mungu alimuita katika eneo hilo.
Je! Wewe ni utumishi upi
unaokuchukua muda mwingi?
4. Uwezo
mkubwa wa Kazi hiyo
Mtu ambaye kaitwa katika eneo
Fulani utaona uwezo mkubwa alionao katika kufanya jambo hilo.
Kutoka 31:1-5,
Mungu anamwambia Musa “ nimemwita
Bezaleli, name nimemjaza Roho ya Mungu, katika hekima na maarifa, na ujuzi na
mambo ya kila aina. Ili abuni kazi za ustadi……….” Bezeleli alikuwa na uwezo
mkubwa katika hekima, maarifa na ujuzi vitu vilivyo onesha dhahili wito wake
kwa Mungu
Matendo 6:7-10.
Stefano alikuwa na uwezo mkubwa
katika kufanya maajabu na ishara kubwa, hii ilionesha wazi wito wake.
Jiulize wewe una uwezo mkubwa
katika kufanya wito upi? Pia inawezekana ukawa na wito zaidi ya moja sio
tatizo, muhimu kila wito Mungu aliouweka ndani yako uutumikie katika viwango
ambavyo vinatakiwa.
5. Matokeo
Mazuri
Kwenye wito huo unaotumika Je!
Unapata matokeo gani? Mazuri au mabaya. Pia unaweza kukapata matokeo mabaya
katika wito ambao ni wako kwasababu tu yakukosa maandalizi, kuishi maisha
yasiyompendeza mungu nk.
Yohana 5:36,
Kazi unazozifanya na matokeo yake
ndizo zikushuhudie kuwa wewe umeitiwa katika eneo gani
Marko 16:15-20,
“Na ishara hizi zitafuatana na…..”
Matokeo ya mazuri ya kazi uliyoifanya ni dalili tosha ya kukujulisha wito wako.
Matendo 8:4-8.
6. Baraka na Mafanikio
Unapokanya wito wako Baraka na
Mafanikio lazima vikuambate
Zaburi 1:3,
“Nae atakuwa kama mti uliopandwa;
kando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake
halinyauki; na kila alitendalo litafanikiwa.”
Mithali 10:22
“Baraka ya bwana hutajirisha, wala
hachanganyi huzuni nayo” Katika eneo ambalo ni wito wako huwezi kuwa na huzuni
bali utaambatana na Baraka tele katika wito huo.
Mith 17:8,
“Kipawa ni kitu cha thamani kwake
yeye aliyenacho, kigeukapo hufanikiwa” kipawa ni wito wa mtu, anasema kila
kigeukapo hufanikiwa”mtu akikifanyia kazi utafanikiwa, utapata mapokeo mazuri
katika wito huo.
7. Ushuhuda
mzuri wa Watu wengine
Math 18:16,
“Zawadi ya mtu humpatia nafasi,
humleta mbele ya wakuu” wito wa mtu unampatia mtu nafasi/kibali katika eneo la
wito wake, kwasababu watu wanaona ni eneo gani ambalo wewe unafanya vizuri.
Yoh 3:1-2,
Nikodemu alimshuhudia Yesu kuwa ni
nani, Alikuwa anaona kilichopo ndani ya Yesu
Mdo 6:1-8.
Mitume alichagua watu saba
watakaosimama kwa ajili ya kutoa huduma kwa wahitaji kulingana na wito wao.
Wito ndani mtu hauwezi kijificha labda mtu mwenyewe asitake kutumika.
Nimeeleza kwa kifupi tu vigengele
kadha vitakavyo kufanya uweze kuutambua kwa haraka wito wako kwa Mungu ili
usigongane na watu wengine katika wito wao. Bila kuzingatia hayo utajikuta kila
siku unatumika chini ya kiwango kwasababu ya kutokaa katika eneo lako mpaka
kufikia hatua ya kuona kama wokovu ni mzigo au hauna faida yoyote.
Mungu anakufundisha ili upate
faida, Usiwe na utumishi usiokuwa na faida yoyote pia ujue namna ya kusimama
katika wito wako
Mungu akutie nguvu katika utumishi
wako
Mungu akubariki sana!
Fuatilia zaidi masomo
haya na mengine katika kitandao ya kijamii kama ifuatavyo;-
Blog: - mungupendo.blobspot.com
Facebook: - Mungu Anakupenda
Youtube: - Mungu Anakupenda
Twitter: - Mungu Anakupenda